Friday, November 12, 2010

CHEKA NA MR.EBBO...NA REMIX YA WIMBO MBADO!

Ule wimbo wa Mr.Ebbo uliovuma sana wakatiule, bado hujaona hivi na vile...kiitikio ilikuwa; mbado. Sasa ameutunga tena kwa remix akisema;

We mtoto si unasema unajua methari? haya basi samaki mkuje....samaki mkunje kama waya!

Oh tunaunda kamati, oh uchunguzi bado unaendelea, oh tunasubiri tume, inaelekea kuwa ni kawimbo ka Taifa sasa, mimi nimeona niwasaidie kurekodi;

Bado hujaona ng'ombe anasunya mtu?....mbado! anakutazama kwa madharau.
Bado hujaona Bajaji imefungwa play?...mbado! yaani wanasikiliza elopi.
Bado huaona mheshimiwa anatembea kama Joti?...mbado! utaanguka uadhirike mheshmiwa.
Bado hujaona nyoka albino?...mbado! waganga vipi analipa?
Bado hujaona jogoo shoga?...mbado! anawika kishoga shoga tu.
Bado hujaona mbwa kauza meno?...mbado! atakuwa ametoka Moshi.
Bado hujaona sokwemtu mchawi?...mbao! analoga loga wenzake porini.
Bado hujaona samaki asiyejua kuogelea?...mbado! yaani wewe kila kitu mbado tu?
Bado hujaona mbwa anatema koozi?...mbado!
Bado hujaona simu za kisasa zinazo tuma harufu mbaya?...mbado! ukinikera tu nakutumia harufu mbaya.
Bado hujaona tumbili ana engachifu?...mbado! huezi jua labda ana mafua.
Bado hujaona mzungu anaimba mipasho (taarabu)?...mbado!
Bado hujaona mtoto wa nyani ananyonya kidole?...mbado! inamkera sana mama yake; hujafia Serengeti wewe.

Tumekubali kuwa kasi mpya, nguvu mpya....ila tu matairi ni ya zamani!

No comments:

WATEMBELEAJI