ELIMU ILENGE ZAIDI KUHUDUMIA ZAWADI YA MAISHA, UTU NA HESHIMA YA MWANADAMU.....
Nawaalika wasomi kuhakikisha kwamba wanatumia vyema elimu yao kwa ajili ya kuhudumia zawadi hii nzuri ya maisha. Kulinda na kuenzi Utu na heshima ya kila mwanadamu, kuishi vyema na wengine hata kama elimu yao ni ndogo au hawakupata kabisa elimu, inabidi kuwaheshimu na kulinda Utu wao. Mara nyingi hutokea wasomi hudharau Utu wa mtu na kusema; mimi siwezi kuongea na asiye soma, kumbuka watu wote Duniani wana umhimu wao, huna budi kuheshimu kazi ya Mwenyezi Mungu kwa kuwaheshimu na kuwajali binadamu wote hata kama hawana elimu ambayo unayo wewe.
Kumbuka kuwa sisi sote ni Binadamu tuna umhimu wa kuishi hapa Duniani.
No comments:
Post a Comment