Monday, November 8, 2010

KATIKA MCHEZO WA MPIRA HAPA ITALY HAIJAWAHI KUTOKEA....

HESHIMA YA MTU NI UTU WAKE SI..... Mchezaji maarufu Eto'o kutoka nchini Camerun, wa timu ya Inter milan ya hapa Italy, akimfunga kamba za viatu golikipa Michele Arcari wa timu ya Brescia, katika mechi ya jana ambapo timu hizi zilitoka droo ya 1-1. Mchezo wakati umesimama kidogo kutokana na mchezaji mmoja wa Inter kuumia, ndipo golikipa huyu alikuwa na viatu vimefunguka kamba zake, aliomba msaada kwenye benchi lake ili wamsaidie kufunga kamba hizo aliwaita, lakini hawakusikia, maana yeye hakuweza kujifunga kutokana na gropsi alizo vaa mikononi. Ndipo mchezaji Eto'o alimsikia na kumwambia nitakufunga mimi, Arcari hakuamini kabisa na kumsifia sana Eto'o, maana katika mchezo huu wa mpira hapa Italy haijawahi kutokea, mchezaji wa timu nyingine kumsaidia kwa namna hii...magazeti mengi yamempa hongera sana Eto'o na kusema hivi ndivo inatakiwa kuwa, katika michezo hii. Jumatano iliyopita Eto'o alialikwa katika kipindi cha TV mmoja ambapo kulikuwa na watoto wadogo wa Kiitaly, walimtwanga maswali mengi ya kuchekesha...aliniacha hoi sana kwa kuyajibu. Hasa yale maswali ya rangi yake nyeusi, alichekesha sana. Mimi nafikiri Eto'o ni mchezaji na ni mtu mzuri katika maisha na sio mpenda makuu, kama wengine tuwaonao. Hongera sana Eto'o ni mfano wa kuigwa hasa kwa Afrika yetu.

Anasema Michele Arcari; Eto'o ni mchezaji maarufu sana, lakini alipiga magoti mbele yangu na kunifunga kamba za viatu, nilibaki mdomo wazi. Ila pia nafurahi sana maana nilimkatalia magoli mengi kwa kupangua mashuti yake, ila alifanikiwa moja kunitundika ( maana goli la Inter lilifungwa na Eto'o mwenyewe, na kwa mwaka huu mpaka sasa anaongoza kwa magoli, mfungaji bora). Ila mengine nilimkatalia na kufanya tutoke droo na timu hii kubwa kama Inter. Maana Brescia ni timu ndogo tu na ukizingatia imepanda daraja la kwanza (Serie A) mwaka huu tu! na inashikilia mkia katika msimamo wa Ligi kuu ya Italy - Serie A.

-Hongera sana Eto'o.

2 comments:

Simon Kitururu said...

Eto'o nahusudu sana mambo zake!

emuthree said...

Safi sana, unaweza ukamsaidia mwenzako kitu kidogo sana, kwake ikawa ni zawadi kubwa sana. Huu ni upendo toka moyoni!

WATEMBELEAJI