Sunday, November 7, 2010

JUMAPILI NJEMA SANA KWENU NINYI NYOTE!

Ee Mungu Mwenyezi Rahimu, utuepushe kwa wema wako na yote yawezayo kutudhuru, tuwe tayari rohoni na mwilini kutimiza mapenzi yako pasipo kizuio.

TAFAKARI YA JUMAPILI;


BWANA NI NGOME YANGU NA WOKOVU WANGU.

Bwana ni Nuru yangu na wokovu wangu nimwogope nani mimi, Bwana ni Ngome yangu na uzima wangu nimwofu nani mimi?
Watesi wangu na adui zangu walijikwaa na wakaanguka kwa uweza wake. Wewe Bwana Mungu wangu, Jeshi lijapo kupigana nami moyo wangu hautaogopa kwa kukutegemea wewe Bwana Mungu wangu. Neno moja tu nalitaka tu! nalitaka kwa Bwana nalo nitalitafuta bila woga wowote.
Nikae nyumbani mwa Bwana siku zote za maisha yangu, niutazame uzuri wa Bwana na kutafakari hekaruni mwake.

-JUMAPILI NJEMA KWENU NINYI NYOTE!

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Nimeipenda tafakari ya leo. Jumapili njema na kwako pia kaka Baraka.

WATEMBELEAJI