Thursday, November 4, 2010

KICHEKESHO CHA LEO!

Mwalimu wa darasa la watoto tahira (Sibusiso - Arusha) alikuwa anawafundisha watoto hao juu ya usafi wakati wa kula matunda. Akisisitiza; Ukipewa tunda ''unaosha, unamenya, unakula'' akawauliza;
Mwalimu; Mkipewa embe?

Watoto; Tunaosha, tunamenya, tunakula.

Mwalimu; Mkipewa ndizi?

Watoto; Tunaosha, tunamenya, tunakula.

Jioni yake akaja Mkuu wa Mkoa kuwatembelea. Maongezi yakawa hivi;

Mkuu wa Mkoa; Nimefurahishwa sana na maendeleo yenu mazuri. Sasa nataka kuwapa zawadi. Je nikiwapa hela mtafanyaje?

Watoto; Tunaosha, tunamenya, tunakula.

Mkuu wa Mkoa....akazirai!!!!

No comments:

WATEMBELEAJI