Thursday, November 18, 2010

KILIMO KIPEWE MSUKUMO WA PEKEE ILI KUTOA UMASKINI WETU!

KILIMO KIPEWE MSUKUMO WA PEKEE ILI KUDHIBITI BAA LA UMASKINI NA UKOSEFU WA AJIRA DUNIANI.


Umuhimu wa kazi katika maisha ya Mwanadamu bila ya kusahau dhamana ya mwanadamu kumshukuru Mungu, kwa matunda ya kazi ya mikono yake. Myumbo wa kiuchumi wa Kimataifa na mkutano wa wakuu wa nchi tajiri al maarufu kama G20, uliomalizika hivi karibuni huko nchini Korea, ni changamoto kwa watu kubadili mfumo wa maendeleo ya kiuchumi Duniani kwa kutoa msukumo wa pekee katika sekta ya Kilimo. Pengo kati ya maskini na tajiri linazidi kuongezeka kiasi cha kupelekea uwepo wa kashfa ya baa la njaa, athari za kiekolojia na tatizo la ukosefu wa fursa za ajira.

Msukumo wa maendeleo ya viwanda kwa miaka mingi yamepelekea kuficha harakati za kukuza sekta ya Kilimo, licha ya juhudi za kuboresha Teknolojia ya Kilimo. Lakini bado sekta ya Kilimo haijapatiwa kipaumbele zaidi cha kutosha hata katika masuala ya kitamaduni. Umefika wakati kwa wadau wote kuwekeza zaidi katika sekta ya Kilimo kwa ajili ya maendeleo endelevu kwa siku za usoni. Juhudi hizi zitajenga katika msingi wa ukarimu, mshikamano, pamoja na ushirikiano katika masuala ya kazi.

Nawapongeza sana vijana wasomi, wanaoamua baada ya masomo yao kujiendeleza katika uboreshaji wa sekta ya Kilimo, si tu kwa ajili ya mahitaji ya mtu binafsi au ya Kifamilia, bali kwa ajili ya mafao ya wengi.

No comments:

WATEMBELEAJI