Thursday, November 18, 2010

SALAMU KUTOKA KWA RAFIKI OLE...WA HUKO TANGA VIJIJINI!

Mh.OLE PICHANI HAPA;Salamu nyingi sana kutoka kwa rafiki yangu Ole, wa huko Tanga katika kijiji cha Kibrashe - Handeni. Nilifahamiana nae huku Italia miaka mitatu iliyopita, alikuwa huku kutokana na kuoana na msichana wa Kiitaly huko Zanzibar waliko fahamiana, na akaja huku ili kuishi na mkewe na baada ya mwaka kupita walifanikiwa kupata mtoto. Lakini kasheshe ilikuwa Ole kuishi huku Ulaya, hakuweza kabisa alikumbuka Tanzania kila siku, na kulia kama mtoto kila kukicha ikawa haiwezekani kabisa kuishi huku. Ndipo mkewe alijaribu kutafuta walau Mtanzania yoyote ili labda ajifariji kidogo, ndipo walinipata mimi na tukafaamiana, ila waliishi mbali na mimi nilipo katika mji wa Genova ni umbali kama wa km 300 kutoka hapa Cesena. Baadae walikuja mara kwa mara kunitembelea, nami nilimfariji Ole lakini ilishindikana kabisa, alisema hawezi kuzoea hata iweje haya maisha si yakwake kabisa! pia alilalama baridi, theruji na watu kutokuwa na uhusiano kabisa mimi haya maisha siwezi, hata kama kwetu ni maskini hatuna mambo waliyo nayo hawa, lakini tuna mambo mengi sana mazuri; alisema Ole. Kwahiyo ikawa ugomvi kila kukicha, maana mke naye alikuwa hataki kwenda kuishi Tanzania, ndipo ikawa mwisho wao hapo....na sasa Ole yupo Tanzania, mkewe na mtoto wapo Italia.

Ole amekuwa rafiki yangu kweli, na mara nyingi ananitumia picha nzuri sana za kimasai kutoka huko kijijini kwake Kibrashe - Handeni - Tanga. Nami nimemwahidi nitakwenda kumtembelea pindi niendapo Tanzania, ili niishi maisha ya kimasai walau hata kidogo, maana mimi napenda sana maisha ya vijijini.

-Asante sana Ole kwa picha nzuri sana za Kimasai.

No comments:

WATEMBELEAJI