Monday, November 29, 2010

MICHEZO MINGINE HAIFAI KABISA.... NI HATARI KWA MAISHA!


Kwakweli michezo mingine ni ya hatari sana katika maisha, mchezo wa kukatisha reli haufai kabisa na ukizingatia treni jinsi zikimbiavyo Ulaya. Kuna wapendanao fulani huko mji wa Milano walikuwa wakicheza mchezo huu hatari wa kukatisha reli, ndipo mauti yalipo mkuta kijana mmoja, baada ya kugongwa na Treni iendayo kasi...hakuweza kuruka wakati treni tayari imeshafika. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 alikufa hapo hapo, na kumwacha mchumba-msichana wake na majonzi makubwa sana, pia kuchanganyikiwa kabisa kutokana na tukio hilo. hata mimi mara nyingi huwa nawaona vijana wengi sana wakicheza karibu sana na reli, na wakati mwingine huwa kunamatangazo kabisa stesheni, ya kuwa watu wakae mbali na reli ni hatari kwa treni ziendazo kasi ambazo huwa hazisimami stesheni zikiendelea na safari. Lakini utakuta vijana wapo karibu tu na kucheza bila wasiwasi, utafikiri maisha kwao hayana thamani yoyote.

No comments:

WATEMBELEAJI