Monday, November 29, 2010

SHILINGI YA TANZANIA KUINGIA KENYA NA UGANDA!!!

Shilingi ya Tanzania itaanza kutumika kama fedha halali katika nchi za Uganda na Kenya, baada ya makubaliano ya pamoja yaliyofikiwa na Serikali za nchi tatu za wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu; alisema Mjini Arusha kuwa wamekubaliana fedha ya kila nchi mwanachama wa EAC kuwa fedha halali kwa malipo ya bidhaa na huduma ya nchi hizo tatu za Afrika Mashariki kuanzia mwezi ujao. Hata hivyo Profesa Ndulu aliongeza kwamba nchi nyingine mbili za Rwanda na Burundi ambazo ni mwanachama wa Jumuiya hiyo zitaongezwa hapo baadae, ingawa hakusema lini.
Tumeamua kuchukua hatua hii muhimu kwa kuruhusu fedha zetu kukubalika katika nchi hizi tatu wakati tukisubiri mchakato ukiendelea wa kupata sarafu moja itakayounganisha nchi wanachama wa Jumuiya hii, alisema; Profesa Ndulu.

No comments:

WATEMBELEAJI