Tuesday, November 16, 2010

NI HATARI SANA KUFUATA NYUMA YA MALORI WAKATI WA SAFARI!

Mwaka huu mwezi wa nane, wakati nikiwa likizo nyumbani Tanzania, wakati tukisafiri tukitokea Singida kwenda Arusha kabla ya kufika Babati katika Kijiji kimoja hivi, tulikuwa nyuma ya Lori moja ambalo lilikuwa na shehena yakutosha. Kuna ki mlima kidogo hivi, lori hilo lilishindwa kupanda na kuanza kurudi nyuma kwa kasi sana, bahati nzuri niligundua mapema pia kutokuwa karibu sana na lori hilo kwa nyuma, nilirudi nyuma kwa kasi na kubaki mbali kuangalia nini kitatokea. Ni hapo kwenye vumbi ulionalo kwenye picha kwa mbali, bahati nzuri utungo wa lori hilo aliweza kuruka kutoka kwenye lori hilo na kuweka kigingi (Kizuio)...ila ilikuwa kazi kweli, maana kigingi cha kwanza lori lilikipandilia halikuweza kusimama, cha pili ndipo lilifauru kusimama. Nilikuwa na wageni vijana kutoka Italia, waliogopa sana na kumsifu sana utingo wa lori hilo kwa kazi aliyo ifanya, kuwezesha lori hilo kusimama bila kuanguka.

- Ndugu zangu madereva tuwe waangalifu sana tunapoendesha magari yetu, tusiyasogelee sana malori kwa ukaribu sana hasa yanapopanda milima, ni hatari sana kwa maisha yetu! tujitahidi sana kuepusha ajali ambazo zingine zinaepukika kabisa, je ningekuwa karibu sana na lori hilo kwa nyuma, ningeweza kweli kuepusha ajali?

No comments:

WATEMBELEAJI