Wednesday, November 17, 2010

NINGEWEZA KWENDA SHULE....NINGELISOMA KWELI KWELI!!!

Mtoto wa Kimasai huko Tanga - Vijijini;

Ningekuwa na uwezo wa kuamua mimi mwenyewe ningekwenda shuleni kusoma vizuri kwa bidii zote, ili hapo baadae niwe; Dokta, Mbunge, Waziri, ikiwezekana hata niwe Rais wa nchi...kwani haiwezekani? Kwanini? mbona Sokoine aliweza??....ila basi tu, Baba ananikataza anasema nikachunge mbuzi na ng'ombe ni mhimu zaidi kuliko shule.
Ningeweza kusoma ili hapo baadae niwe mkombozi wa Taifa langu la Tanzania. Haya basi ngoja nikachunge mbuzi wangu kwasasa, baadae tutaona, Baba akija kuamua kunipeleka shule!

No comments:

WATEMBELEAJI