Wednesday, November 17, 2010

T-SHIRT YA MWIMBAJI MAARUFU WA ITALIA YALETA GUMZO...

Mwimbaji maarufu wa Italia, Gianna Nannini, ambaye pia ni mjamzito kwasasa, kama aonekanavyo hapo...alionekana amevaa nguo hii iliyoandikwa; GOD IS A WOMAN. Amewakwaza watu wengi sana, hata wengine ni wapenzi wake sana, lakini wamechukizwa na kitendo hiki cha kuvaa nguo hii ya maneno haya. Pia nchini Vatican kwa Papa mwenyewe hawajalichukulia vizuri swala hili.

Kwakweli nimeamini binadamu lazima tuwe waangalifu sana kwa yote tufanyayo, maana unaweza ukawa na wapenzi na wafusi wako wengi sana, lakini ukikosea kidogo tu hata kwa kuvaa nguo yenye maneno yasio mazuri, unaweza kupoteza kila kitu kilicho kizuri na cha maana kwako, kwa maswala madogo tu kama haya. Kwakweli watu wengi limewakera sana jambo hili.

No comments:

WATEMBELEAJI