Sunday, November 14, 2010

UPIKAJI WA CHUMVI KATIKA KIJIJI CHA KINANGALI - MANYONI.


Barabara ya kwenda kwenye chumvi katika Kijiji cha Kinangali. Hapa tuonavyo hata mtoto mdogo kabisa anasaidia katika ubebaji wa kuni kwaajili ya kupikia chumvi, mama naye akiwa na maji kichwani kwaajili ya kazi hiyo. Umbali kutoka kijijini hapo mpaka kufika mbugani kwenye chumvi unatisha sana, lakini wenyewe wamezoea sana mpaka kukataa hata lifti yetu kwenye gari, kwakweli maisha yetu haya bado tupo mbali sana....lakini basi ndo maisha yetu haya hatuna jinsi. Ila inasikitisha sana...kwanini wengine wanaishi kwa raha zao na wengine kila kukicha ni tabu tu?

Hapa ndipo kwenye chumvi penyewe, kutokana na umbali kutoka Kijijini hadi mbugani, wapikaji chumvi huamua kuhamia hapo hapo ili kufanya kazi zaidi, na hulala kwenye viduara hivyo vya majani, kama tuonavyo hapo kwenye picha. Kazi ngumu kweli hii, pia ukizingatia haina soko kabisa...wanadhurumiwa sana kwa kazi yao hii kubwa, wafanyabiashara wanakuja kununua kwa bei nafuu mpaka debe sh.1000, wanasema kama hutaki acha nitanunua kwa mwingine...mpaka huzuni kabisa! Kwasababu hakuna mtu au kiongozi yoyote anaye jihusisha kuwasaidia kutafuta soko na kuwatetea kwa hali na mali.


Hapa ndipo upikaji wa chumvi unafanyika, ni kuungua na mto haswa, jua kwa sana, kuni kuzipata si mchezo umbali wake balaa....maji ya shida, yaani we acha tu!



No comments:

WATEMBELEAJI