Lumbesa hii, hata kama ni majani....lakini ni lumbesa tu! Usifikiri ni Bongo - Tanzania kwenye mahangaiko yote, hata kwa wenzetu sehemu mbalimbali za Dunia hii kuna tabu na shida zake. Vijana wengi Tanzania huwa wananiuliza na kuamini kuwa huku kwa wenzetu hakuna kabisa shida, mimi huwa nikiwajibu shida na matatizo yapo sehemu zote Duniani, huwa ni ugomvi hawataki kuamini na kusema wewe hutaki tuende na sisi huko. Kumbe hawajui kuwa huku huwezi kumwomba hata chumvi tu jirani yako, na majirani mnaishi milango inaangaliana, mnaishi miaka nenda rudi hamfahamiani kabisa.
Mimi nataka kutoa ujumbe kwa vijana wote wa Tanzania kuwa maisha si Ulaya au sijui wapi...maisha ni kujituma kwabidii tu! utafanikiwa na kuwa na maisha bora sana ukiwa hapo hapo Tanzania. Mbona mimi nawafahamu vijana wengi tu wana maisha mazuri sana kushinda hata mimi niliopo Ulaya, hawajaenda Ulaya wala sehemu yoyote zaidi ya Tanzania, na tena hata ukiwalipia nauli ya kwenda Ulaya hawata kubali kabisa. Maisha ni popote tu! upatapo kazi au biashara ujitume kwa bidii zote na kwa malengo mazuri, hata kwa kile kidogo ukipatacho....ipo siku tu utafanikiwa tu!
No comments:
Post a Comment