Saturday, November 13, 2010

WANYATURU WAMPONGEZA MH.MOHAMMED DEWJI.

Mh.Mohammed Dewji, aka MO Mbunge wa Singida, akipongezwa na wapiga kura wake. Mh.Mohammed Dewji, pamoja na mkewe wakiwa wakitabasamu kwa furaha kabisa, baada ya kuvalishwa mavazi ya asili ya Wanyaturu...watu wa Singida, jana baada ya kuapishwa wakiwa nje ya viwanja vya Bunge - Dodoma.
Mke wa Mh.Dewji, pia alipata fursa ya kuvalishwa vazi la asili la Mkoa huo wa Singida, kama unavyoona pichani akiwa amebebeshwa kibuyu na wamama wa Singida.

Kikundi cha ngoma kinachojulikana kama Misaki, kikitoa burudani viwanja vya Bunge - Dodoma.


Mh.Mo, akimsikiliza kwa makini mwenyekiti wa kikundi cha ngoma, Mwajuma Jumanne, alipokuwa akimkabidhi kibuyu ambacho ndani yake kilikuwa na karanga, katika sherehe hiyo ya kumpongeza Mh.Mo, zilizofanyika kwenye Hotel ya Kitemba iliyopo Mjini Dodoma.



No comments:

WATEMBELEAJI