Wednesday, December 1, 2010

KIJIJI CHA MATUMAINI CHA DODOMA NA WAGOJWA WA UKIMWI!


KIJIJI CHA MATUMAINI CHA DODOMA NI MFANO WA KUIGWA KATIKA KUWAHUDUMIA WAATHIRIKA WA UGONJWA WA UKIMWI.
Taasisi ya Kijiji cha Matumaini, iliyoko Jimbo katoliki Dodoma, Tanzania...imekuwa mstari wa mbele katika kuwahudumia wagonjwa na waathirika wa Ukimwi, kwa kutoa huduma kwa watoto yatima na walioathirika kwa Ukimwi. Huduma ambayo imepanuliwa ili kuwawezesha hata wagonjwa watokao nje ya kijiji hicho kufaidika.
Katika mahojiano maalum na Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican, Padre Vincent Boselli - CPPS, muasisi wa Kijiji cha Matumaini alisema; walau kila mwenzi kuna wagonjwa wapya kati ya 20 hadi 30 wanajitokeza ili kupatiwa huduma ya dawa za kurefusha maisha.
Kwasasa Kijiji cha Matumaini kinawahudumia wagonjwa zaidi ya 2500 kutoka nje ya Kijiji hicho, changamoto kwa watu kubadili tabia, kuwa waaminifu na kujizuia, vinginevyo ugonjwa wa Ukimwi utaendelea kufyeka maisha ya watu wengi zaidi Duniani. Kumekuwepo na ushirikiano mzuri kati ya Kijiji cha Matumaini na Wizara ya Afya katika huduma kwa waathirika wa ugonjwa wa Ukimwi, lakini Kijiji cha Matumaini kama taasisi bado inabeba dhamana na mzigo mkubwa zaidi katika kuwahudumia waathirika wa ungojwa wa Ukimwi, wangependa kutoa huduma hii kwa kila mtu anayepiga hodi hapo, lakini hali halisi ya uchumi na upatikanaji wa dawa zinazohitajika unakwamisha ndoto kama hii.
Kijiji cha Matumaini kimekuwa na mvuto mkubwa kwa waathirika wa ugonjwa huu wa Ukimwi, alisema Padre Boselli; kutokana na huduma bora ya tiba ya kurefusha maisha. Mazingira safi, lakini zaidi ni ile thamani, heshima na utu wa kila mgonjwa, kwani ndani yake wao wanamwona Kristo mteseka anayehitaji kuhudumiwa kwa moyo wa upendo na ukarimu zaidi.
-Vijana na watu wote tujihadhari na gonjwa hili baya la Ukimwi.

No comments:

WATEMBELEAJI