Friday, December 3, 2010

KILA NIENDAPO MBUGA ZA WANYAMA LAZIMA NIUGUE......

......Kwa vyakula vyao hivi vya Box, sikui kwanini huwa napata shida sana na hivi vyakula, ila mwaka huu nilisikia hata watu wengine pia wakilalamika kuhusu hizi Box. Mimi nafikiri upikaji wao si mzuri. Mimi lazima niugue kabisa sio tumbo tu peke yake mpaka homa juu. Kwa wageni sio vizuri sana mambo haya, kwanini jamaa nyie wa Utalii msifuatilie hili jambo na litafutiwe ufumbuzi wake? maana wageni wengi sana wanalalamika sana na hizi chakula za Box. Leo tu nilikuwa nasoma gazeti fulani la hapa, jamaa mmoja akitoa moja ya sifa mbaya za utalii Tanzania ni hili swala la chakula hiki cha Box. Jaribuni kuangalia swala hili, tusije tukaharibu biashara yetu ya utalii na swala dogo tu! Tukumbuke kuwa Watalii hawana dogo.

No comments:

WATEMBELEAJI