Wednesday, December 8, 2010

LEO ILIKUWA SIKUKUU YANGUY X-MAS HAPA CESENA-ITALIA....







.....Nasema hivi kuwa ni sikukuu yangu ya X-mas kwa hapa mji niishipo Cesena, kwasababu nimeagwa na maraiki zangu ambao ningekuwa nao kwa vyovyote vile katika sikukuu hii yaX-mas, lakini basi sitaweza kuwa nao kwasababu....naondoka kesho usiku kuelekea nyumbani Tanzania kwa likizo na mambo mbalimbali madogo madogo ya kikazi. Nifuraha sana kwangu kuwa nyumbani kwa sikukuu ya X-mas na Mwaka mpya, baada ya muda mrefu kuto uhudhuria sikukuu hizi nikiwa nje ya nchi. Pia ni furaha sana kurudi kwetu, hata kama ni muda mfupi nilikuwa huko mwezi wa Tisa mwaka huu.....lakini ni furaha ilioje.
Pia napenda kuwaaga wadau wangu wote wa kijiwe hiki cha KAZI YAKO NI JINA LAKO. Naamini tutakuwa pamoja daima kwa sikukuu hizi zote mbili, hata kama nitakuwa huko Tanzania nitakuwepo nanyi daima kuendeleza libeneke, ila kama mnavyofahamu mitandao ya kwetu huwa inasumbua sana, mara umeme wa mgao n.k, lakini nitajitahidi sana kwa nguvu zangu zote kuwa nanyi kwa kuwaleteeni habari na mambo mbalimbali kama kawaida.
Asanteni sana tupo pamoja daima.



No comments:

WATEMBELEAJI