Wednesday, December 8, 2010

MILIMA MIREFU UNAPUNGUZA KASI YA GONJWA LA KANSA!

Nilikuwa nikipitia pitia magazeti kama kawaida kila siku ndipo nilipo kutana na gazeti hili, ambalo lina habari ya huyu mwana Mama Martina Navratilova, miaka 54 ambaye alikua mcheza Tenes maarufu. Na kwasasa ana ugonjwa wa kansa, ndipo alipo shauriwa apande Mlima wa Kilimanjaro...inasaidia sana kama moja ya matibabu ya ugonjwa wake huo. Mwana Mama huyu kwa muda ameishi Kenya, na kwasasa ameamua kuhamia Tanzania na kufanya matembezi yake ya kupanda Milima Kilimanjaro. Alianza safari yake hiyo ya kuupanda Mlima Kilimanjaro tarehe 6/12/2010 pamoja na watalii wapanda milima wapatao 28 kutoka sehemu mbalimbali za Dunia hii. Wataalamu wanasema inasaidia sana hewa ya juu ya Milima mirefu katika gonjwa hili la kansa.

-Kila lakheri kwa wagonjwa wote wa kansa, pia Martina.. na upandaji mwema sana wa Mlima wa Kimanjaro.

No comments:

WATEMBELEAJI