Friday, December 3, 2010

WANACHUO NA UJUMBE WAO KWA WAZIRI MKUU WA ITALIA....

......Ujumbe wa wanafunzi wa chuo wa hapa Italy, kwa Waziri Mkuu SILVIO BERLUSCONI. Wakisema; Silvio una nywele hizo ulizo nazo.... yote hayo ni asante kwa Utafiti!

-Maana Waziri Mkuu Silvio ana nywele za kutengeneza kwa utaalamu sana mpaka huwezi kugundua. La sivyo angelikuwa na kipara cha kufa mtu.

Sasa habari yenyewe ni hivi; Serikali iliamua kukata sana kwa kupunguza sana fungu la utafiti, ndipo wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya hapa Italy waliamua kugoma kabisa kwa siku kadhaa...kugomea swala hilo na kusema kwa pamoja utafiti ni muhimu sana kwa Dunia ya sasa, kwanini sasa Serikali inapunguza fungu kwa ajili ya mambo kama hayo? Ndipo wanafunzi hao katika miji mbalimbali ya hapa Italy waliamua kugoma na kwenda mabarabarani na mabango mbalimbali na kwa fujo mbalimbali....moja wapo likiwepo bango hili kwaajili ya ujumbe kwa Waziri Mkuu Berlusconi.

No comments:

WATEMBELEAJI