Friday, February 4, 2011

FEDERICA TREGNAGO....NA FURAHA YAKE YA TANZANIA!

Mdada Federica Tregnago kutoka Verona - Italia, na furaha yake alivyokuwa Miyuji - Dodoma -Tanzania. Ameandika maneno mazuri sana katika ukurasa wake wa Facebook, anasema Tanzania imembadilisha sana katika maisha yake, amekuwa mwenye upendo mwingi na furaha sana moyoni...ambapo hakuwa hivyo mwanzo, amekutana na watu (Watanzania) wenye upendo hajapata kuona kabisa, mpaka kufanyiwa Birthday yake kwa shangwe hajapata kuona upendo huo, sifa nyingi sana katumwagia sisi Watanzania. Yeye na wenzake wawili walikwenda Miyuji - Dodoma kusaidia kazi mbalimbali katika kituo cha watoto walemavu wa akili, wanasema hawakubali kabisa lazima warudi tena baada ya kumaliza masomo yako. Hasa yeye Federica amepania sana!


Federica mwenye miwani, na wenzake Sara na Elisabeth...wakiwa Miyuji - Dodoma!


Katika kazi ngumu ya kuchimba mtaro.



Miyuji Cheshire Home- Dodoma - Tanzania.







Hapa ni Video ya Birthday ya miaka 25 ya Federica.

Federica dice;
Che mai avrei potuto immaginare, che mai dimenticherò e che è stata davvero stupenda....ricchissima di emozioni!!! Bella bella...uno dei 40 giorni memorabili passati a Miyuji - Dodoma - Tanzania.
Questo video riesce sempre a strapparmi un sorriso.
KWA KISWAHILI:
Federica anasema;
Daima sikutegemea, daima sitasahau uzuri uliotokea....utajili wa emosheni!!! Nzuri nzuri...siku kati ya siku 40 ambayo sita isahau kati ya siku nilizo kaa Miyuji - Dodoma - Tanzania.
Video hii inaniwezesha daima kutoa tabasamu.

No comments:

WATEMBELEAJI