Thursday, February 17, 2011

MJASIRIMALI AKISAFIRISHA MATENGA YA NDIZI!

Mjasirimali; Joseph Damas....akisafirisha matenga ya ndizi, moja likiwa kwenye baiskeli na jingine akiwa kalibeba kichwani.
Damas alikuwa akitoka milima ya Uluguru, akipeleka mzigo huo kwenye genge lake huko Kihonda kwa Chambo, umbali wa kilomita kumi.

-Kwakweli tuna maisha magumu kweli, yaani mpaka basi. Mimi binafsi ningependa sana viongozi wetu hata wao wafanye kazi kama hizi kwa miezi mitatu mfululizo, baada ya hapo naamini wangetupa majibu vizuri zaidi kuhusu vipato vya wananchi viweje na maisha yao yaweje. Utakuta mtu kama huyu anahangaika hivi pia atanyanyaswa na maswala ya kodi, kulipia ushuru wa genge lake, kweli ni haki hii???

No comments:

WATEMBELEAJI