Wakati nikiwa likizo nyumbani Tanzania, Januari 2011. Nilipatwa na hamu sana ya kukumbushia kazi yangu ya zamani ya uchimbaji visima. Nilifurahi sana kupata nafasi hiyo tena...walau kwa muda mfupi, lakini kulinifurahisha sana moyo na kutamani sana kurudi tena moja kwa moja katika kazi hizo za kusaka maji, hasa kwenye shida sana ya maji huko vijijini. Ni kazi ngumu sana inahitaji uvumilivu wa hali ya juu, hasa huko vijijini maporini....unakosa kila kitu, mahitaji mhimu kwa muda usio eleweka mpaka kisima kikamilike si mchezo, wakati mwingine visima vingine vinasumbua sana inabidi kubaki kwa muda mrefu ili kukikamilisha vizuri. Kama hiki tulichimba kwa shida sana, kutokana na kubomokea ndani, aridhi yake ni nyepesi sana, ukikuta mwamba mgumu huwa ni rahisi, pia upande mwingine ni vigumu maana inabidi kubadili kila mara biti ya kuchimbia kutokana na makali kuisha mapema kutokana na mwamba mgumu. Hapa nilienda nao baada ya mwaka mpya kupita, tulikuwa katika pori la Itigi....nje kidogo mwa mji huo wa Itigi, katika Wilaya ya Manyoni, Mkoani Singida. Nilifurahi sana na ipo siku nitarudi moja kwa moja katika kazi hii ya kutoa huduma kwa wenye shida ya maji.
-KAZI YAKO NI JINA LAKO.
No comments:
Post a Comment