Wednesday, March 9, 2011

IBADA YA MAJIVU ..... TUBUNI NA KUIAMINI INJILI!

MWANADAMU KUMBUKA KUWA U MAVUMBI WEWE, NA MAVUMBINI UTARUDI!
Askofu Severene Niwemugiza wa Jimbo la Lulenge, akiwapaka majivu ikiwa ni ishara ya kuanza kwa kipindi cha mfungo wa kwaresima, Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda na mkewe Mama Tunu Pinda, katika Ibada fupi iliyofanyika katika makazi ya Askofu, mapema leo Machi 9, 2011. Mh.Pinda yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Kagera.
- Tugeuze mwenendo wetu kwa majivu na gunia tufunge na kulia mbele ya Bwana, kwa maana Mungu wetu ni mwingi wa rehema, naye hutusamehe dhambi zetu. Tugeuze mwenendo wetu, tufanye vema zaidi mambo tuliyokosa kwa ujinga, isije ikawa tunapotafuta nafasi ya kutubu tusiweze kuipata, tukafikiwa ghafula na siku ya kufa.
*Sikiliza ee Bwana, uturehemu sisi, kwa kuwa tumetenda dhambi mbele yako.*

No comments:

WATEMBELEAJI