Ee Bwana, utujalie sisi sote waamini wako tuanze vita vya Roho kwa mfungo mtakatifu. Nasi tulio tayari kupigana na pepo wabaya tujipatie nguvu kwa sababu ya kufunga.
Ee Bwana, wewe wavipenda vitu vyote vilivyopo, wala hukichukii kitu chochote ulichokiumba. Unawasamehe watu dhambi zao kwa ajili ya kufanya kitubio na kuwahurumia kwa kuwa ndiwe Bwana Mungu wetu.
Ee Mungu wetu, uturehemu sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, uyafute makosa yetu, uyaoshe kabisa na uovu wetu na uzitakase dhambi zetu.
Kwaresima ni kipindi cha mapambano ya maisha ya Kiroho, tujivike silaha za fadhili za Kikristu. Tujifunze maana ya mateso ya Kristu, ili kukuza na kuimarisha Imani, maadili na Utu wema kwa njia ya ushuhuda wa maisha.
TUTUBU NA KUIAMINI INJILI; KWARESIMA NJEMA KWENU NINYI NYOTE!
No comments:
Post a Comment