Tuesday, March 8, 2011

KATIKA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

WAWEZESHENI WANAWAKE NA WASICHANA KWA KUWAPATIA FURSA SAWA YA ELIMU.Leo ni siku ya wanawake Duniani kote. Ni siku inayowakumbusha wanawake wa Dunia hii umuhimu wao wa kuendeleza mapambano ya kujikomboa. Ni siku pia inayotukumbusha hata sisi wanaume wajibu wetu kwa wanawake na familia zetu. Na kama kweli unampenda umpendaye basi umjali na kumtunza ni pamoja na kushirikiana majukumu ya kifamilia ikiwemo kulea watoto.

Umuhimu wa kuwawezesha wanawake katika elimu; ili waweze kuboresha maisha yao, familia zao na Jamii inayowazunguka...kwa kulinda na kudumisha Utu na Heshima ya Mwanadamu, ambazo ni Tunu msingi za Kiroho na Kiutamaduni.
Haya ni kati ya mambo ambayo Taasisi za Elimu zinapaswa kuzingatia wakati wa utoaji wa Elimu, inayopania kumletea mwanadamu ukombozi wa kweli katika maisha. Ikiwa kama mambo haya msingi yatakosekana kuna hatari kwamba; Elimu haitaweza kufikia lengo linalokusudiwa na kuleta mwanga mpya katika maisha ya watu.
Umuhimu wa kuzingatia sheria asilia ambayo kimsingi ni Urithi wa mwanadamu katika utekelezaji wa mikakati ya Elimu, inayopania kuwawezesha watu kutambua mafao ya wengi, ili ili kuyafanyia kazi mabaya yanayo kwamisha maendeleo endelevu ya mwanadamu kuyaweka kando. Elimu ni msingi inapaswa kufumbatwa kwa namna ya pekee mang'amuzi yanayo wawezesha wazazi na walezi kuwa kweli ni wadau wakuu katika majiundo ya watoto wao.

Wanawake wanapaswa kupata fursa ya Elimu, Ajira na mapato halali kwa kazi wanazo zifanya bila ya ubaguzi wa kijinsia. Yote haya yafanyike kwa lengo la kukuza na kuimarisha mafao ya wengi ndani ya Jamii. Taratibu na kanuni za kazi ziwawezeshe wanawake kutekeleza majukumu yao ndani ya familia na Jamii kwa ujumla, mintarafu uwezo wao wa kimama. Wanawake wanaoishi katika maisha ya ndoa na familia wanapaswa pia kusaidiwa kwa hali na mali, kwani familia ni chimbuko la jamii.


LUCK DUBE.......GOD BLESS THE WOMAN.

HAPPY WOMAN'S DAY!

No comments:

WATEMBELEAJI