Mungu wetu mwenye nguvu ni Baba wa milele yote, watupa mema mengi... wewe ni mwenye nguvu pekee tena ni wa milele.
Nguvu zako zashangaza sana hii Dunia, uliumba mbingu kwa wema na kutupenda sana sisi wanadamu. Matendo yako ya ajabu sana, neema yako na fadhili zako kila asubuhi ni mpya tena za tufariji sana mioyo yetu kila tuamkapo. Tukikosewa na haya maisha watupa tumaini lako la kupata maisha mapya, wajapo tucheka majirani zetu...wewe upo upande wetu; uhimidiwe daima Mungu wetu!
Wanipa tumaini la maisha hapa Duniani, natembea nawe Baba yangu hujaniacha kabisa mimi, kulala na kuamka kwangu mimi ni kwa neema yako Mungu wangu. Ulimpa nini Mungu ili uwe hivyo ulivyo....usijivune kabisa maana yote ni neema anazo kupatia Mungu.
Nani kama wewe Bwana? Sina mwingine wa kujivunia zaidi yako wewe, wewe ni mwanzo na mwisho Baba. Utukuzwe daima, uhimidiwe daima Baba.
-Nitakusifu na kukutukuza daima katika maisha yangu yote....kupitia binadamu wenzangu; kwa kuwapenda, kuwaheshimu na kuwajali daima!
No comments:
Post a Comment