Sunday, May 22, 2011

MANENO MAZURI YA JUMAPILI HII YA 5 YA PASKA!

Mwimbieni Bwana wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu; machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake.....aleluya!


Ee Mungu wetu mpendwa, umetuletea ukombozi na kutufanya watoto wako...tunakuomba sana utusikilize kwa wema wako sisi wanao, ili katika kumwamini Kristu tupate uhuru wa kweli na urithi wa milele.

Ee Mungu wetu mpendwa; umetushirikisha Umungu wako mkuu katika kushiriki sadaka hii Takatifu, tunakuomba utujalie kuufuata kwa mwenendo mwema ule ukweli wako kama tunavyojua.


Bwana asema; Mimi ndimi mzabibu wa kweli, nanyi ni matawi.....akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana.....aleluya!

No comments:

WATEMBELEAJI