Sunday, May 22, 2011

JUMAPILI NJEMA SANA KWENU NINYI NYOTE WADAU WANGU!



KATIKA MWEZI HUU WA BIKIRA MARIA MAMA YETU MPENDWA SANA; MAMA WA ROZARI! TAFAKARI YANGU YA LEO NI;


Mama yetu mpendwa sana Bikira Maria, Mama mtetezi wa wanyonge Maria.....msaada wa Wakristu na kimbilio letu sote; Maria msimamizi wetu sote utulinde na kutuongoza katika haya maisha. Ulinde Jumuiya zetu, Parokia zetu, na Majimbo yetu, ili yaongoze watu vizuri katika sala na upendo dhidi ya Mwenyezi Mungu; kwa upendo wa mapendo ya kupendana sisi kwa sisi ili siku moja tufike mbinguni ulipo wewe Mama yetu mpendwa sana! Ongoza Kanisa letu, pia viongozi wetu.. wajalie afya njema ya mwili pia ya roho, pia waumini wote...akina Baba na Mama na Watoto wote, pokea karama zetu uende kwa unyoofu! Waombee Maaskofu, Mapadri na Watawa wote waihubiri Injili ipasavyo hata mwisho wa dahari....Tuombee kwa Mwanao Yesu Kristu, atuepushie dhambi na atufikishe Mbinguni tufurahi siku zote, amina!


No comments:

WATEMBELEAJI