Thursday, June 30, 2011

AIRPORT YA ADDIS ABABA - ETHIOPIA.







Mambo ya wenzetu haya mpaka basi. Roho huwa inaniuma sana sisi tu tunashindwa kuimarisha hata vitu muhimu kama Airport ambayo inatuingizia sana hela, sasa sijui ni kwanini? Nimepita hapa Ephiopia nimeona mambo yalivyo mazuri hadi barabara za juu wanazo, sisi kwanini tusiweze? Nenda Nairobi tu! ambao tupo nao jirani utaone kama panafanana na Dar es salaam. Ndege zetu za Taifa zimetushinda kabisa, wenzetu wana mabege mpaka basi, ndo haya tunasafiri nayo mpaka Ulaya. Hivi kwanini hatuoni aibu jamani?





1 comment:

Anonymous said...

Mzee Chibiriti bora umeliona nahisi wale watu wanao husika na uwanja wa ndege wetu akili zao zimejaa utindio wa hali ya juu sana, hawawezi jifunza kitu hata siku moja uwanja wa ndege una giza kama nini, sehemu ya kukaaa ni shida pia basi tuu tuombe mungu.\


Mdau wako

BEN -SOUTH KOREA

WATEMBELEAJI