Kila nipitapo hapa lazima nisimame na kupiga picha, labda niwe kwenye basi...lakini kama ni usafiri wangu binafsi lazima nisimame. Ni jiwe ambalo huwa linanivutia sana jinsi lilivyokaa, pia lilivyo lenyewe. Ipo siku nimepanga nilipande mpaka juu kwa utundu wangu nilionao wa kukwea kila kitu kilicho kwenda angani, ipo siku yake tu! Kila nipitapo hapa huwa nakuwa na watu waoga wananikataza sana, nakusema; ni hatari ni hatari! siku nikipata watu wa kunisapoti lazima nilipande tu!
Jiwe hili lipo katika barabara kuu ya Dodoma - Singida, ukitokea Dodoma unaenda Singida kabla hujafika Bahi, lazima ulione tu! Nikiwa na wageni wangu wa kizungu hata wao huwa wanachanganyikiwa wakiliona hili jiwe, kwakweli Tanzania tuna utalii mwingi sana ila hatujui kabisa kuutumia.
No comments:
Post a Comment