Sunday, June 26, 2011

JUMAPILI NJEMA SANA KWENU NINYI NYOTE WADAU WANGU!



TAFAKARI YANGU BINAFSI KATIKA JUMAPILI HII;


- Matumaini ya safari yetu sasa yameingia dosari, kwani meli tuliyopanda kuja kwako Bwana wetu....tazama imevamiwa na majambazi. Hakuna njia nyingine itakayotuokoa kwenye janga hili, Yesu mwema njoo haraka utuokoe wanao tunakwisha wote; Gonjwa hatari lisilo tibika ona linatumaliza wote, halichagui, halibagui....linafyeka tu! gonjwa hilo ni ukimwi halina huruma kwa wanadamu, limeuwa watu wengi wakubwa kwa wadogo wamepotea, milenia tuliyomaliza ilijaa huzuni, majonzi kila upande! Wana Sayansi, Madaktari wanahangaika kutwa kucha...juhudi zinagonga mwamba hakuna dawa...ee Bwana tunakufa tuonee huruma, tunakuomba Mungu Mwenyezi ingilia kati kwa uwezo wako wote. Macho yao uyafungue, fanaka ipatikane ee Bwana tunakuomba!


Tumeshaomba tumesali sana ee Bwana sikia sala zetu, tunaungama tumekosa ee Mungu Mwenyezi....tazama tunakulilia tusikilize, tunakufa kama nzige ee Mungu tunateketea wote....si Sodoma wala Gomora, jamaa hili linazidi tena linatisha. Ee Yesu mwema mwenye huruma tunakuomba ututazame; damu na maji vilivyotoka moyoni mwako vilete dawa harisi ya kutuponya! Watoto ni wengi sana wanakufa bila hatia yoyote inasikitisha sana, wengine sasa ni yatima hawajui wataishi vipi maisha yao. Tunakuomba ee Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho Mtakatifu; Milenia tulioianza njoo Bwana utawale mioyo yetu, machozi tunayolia yafute maovu yetu yote kwa mema yako....lakini mapenzi yako yatimizwe vile utakavyo, tunakushukuru!

No comments:

WATEMBELEAJI