Enzi hizo; hapa ni Parokiani Tegeta - Dar, nikiwa na Watumikizi wenzangu kabla ya misa kuanza...tukijiandaa, mimi nilikuwa napenda sana kupiga chetezo, ikifika zamu yangu nilikuwa nafurahi sana! Huniambii kitu hapo.
Enzi hizo Parokiani Tegeta, moja ya misa za Askofu Pengo; tukitumikia Misa ya Askofu Pengo, ambapo sasahivi ni Kardinali. Mimi ni wapili kutoka huyo wa kwanza anayeonekana upande wa kushoto. Tukiongozwa na watoto wakicheza na kuimba kwa furaha!
Enzi hizo Parokiani Tegeta, nikiwa pamoja na kikosi kamili cha Watumishi. Wa kwanza kushoto mwenyenguo nyeupe zote (kwa jina Pambano).. sasahivi ni marehemu baada ya kupata ajali mbaya ya gari, miaka minne iliyopita akiwa Mwanajeshi hapo Dar. Mungu ailaze Roho ya Marehemu Pambano...mahali pema peponi - Amina!

Nilikuwa napenda sana kutumikia misa, pia kupata mafundisho ya dini nilikuwa sikosi, na Parokia zangu ni mbili, kati ya Kijijini na Tegeta ndipo nimekulia sehemu hizi mbili, kutokana na Mama yangu kuhamishiwa Dar katika kumfuta Baba kwa mambo ya ki kazi. Mimi nilikataa kabisa kuhama Mjini, na waliondoka waliniacha huko Kijijini nikiwa darasa la nne...hivyo nilikuwa nikienda wakati wa likizo ya shule kufungwa, nilikuwa napenda sana Kijijini hadi mpaka sasa maisha yangu zaidi napenda kuishi Kijijini. Pia nilipokuwa mtoto nilikuwa na ndoto sana ya kuwa Padri, lakini baadae nilibadili mawazo na kuona sio njia yangu...hivyo sipaswi kulazimisha. Lakini yote namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa maisha mazuri aliyonipatia...na anaendelea kunipatia mpaka sasa, pia namwomba sana anipatie Familia njema yenye kumweshimu yeye daima!
No comments:
Post a Comment