Sunday, June 26, 2011

MANENO MAZURI YA JUMAPILI HII.

JUMAPILI HII YA MWILI NA DAMU TAKATIFU YA BWANA WETU YESU KRISTU!


Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu; kwa kutuamuru hivyo Kristu alitaka sisi tuadhimishe fumbo hili la Mwili na Damu yake mpaka atakaporudi. Katika sikukuu hii tunafanya tena ukumbusho wa karamu ya mwisho, tunapoadhimisha hii siku ya paska...yaani Alhamisi Kuu jioni, hatukuweza kufanya hivyo kwa shangwe kwasababu ya kukumbuka mateso ya Kristu. Kwahiyo Kanisa hurudia leo adhimisho hilo likimshangilia na kumshukuru Kristu hasa kwa maandamano kwaajili ya zawadi hii kubwa. Zawadi hii ni Mwili na Damu yake mwenyewe inayotukumbusha kufa na kufufuka kwake na pia ni chakula chetu cha roho.


Nimewalisha kwa unono wa ngano na kuwashibisha kwa asali itokayo mwambani.

Ee Mungu, umetuachia ukumbusho wa mateso yako katika Sakramenti ya ajabu. Tunakuomba utujalie kuyaheshimu mafumbo matakatifu ya Mwili na Damu yako, tupate daima neema ya ukombozi wako ndani yetu. Unayeishi na kutawala pamoja na Mungu Baba....daima na milele - amina!

Bwana asema; aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu...hukaa ndani yangu, nami ndani yake.

No comments:

WATEMBELEAJI