Thursday, June 2, 2011

TAFAKARI KWANZA....KABLA YA KUOVATEKI!



Nilipokuwa shule ya udereva...mwalimu alikuwa akisisitiza sana na kusema; tafakari kwanza vizuri na uwe na uhakika kweli, kabla hujaanza kuovateki ( kumpita mwenzako). Pia alikuwa anasema; kumbuka kuwa duniani madereva ni wachache sana, ila waendeshaji magari ni wengi sana, kweli nimeamini alikuwa akisema ya kweli, dereva wa kweli kweli hawezi kabisa kufanya hivi afanyavyo huyu hapa kwenye picha...ikitokea ajali, aaa...!!!! ni bahati mbaya tu au ni mipango ya Mungu, hakuna kitu kama hicho...ni uzembe mkubwa sana wa watu kama hawa, wanauwa watu wasio na hatia yoyote. Kweli kuna ajali huwa zinatokea unaweza kabisa kusema bahati mbaya, sasa huyu je naye ni bahati mbaya?

Jamani tukiwa barabarani tuwe makini, sio tu tunahatarisha maisha yetu bali maisha ya wenzetu wengi, ukifa wewe tu peke yako na ujinga wako...hamna shida, lakini pale unapohatarisha na kukatisha maisha ya wenzako hasa ya wale watoto wadogo, vijana taifa la kesho.....kwakweli unastahili adhabu kubwa sana.

-TAFAKARI KABLA YA KUOVATEKI.....NI MUHIMU SANA, NA MARA NYINGI AJALI NYINGI NDIPO ZINAPO TOKEA, CHANZO KIKUBWA CHA AJALI HIZI ZA BARABARANI NI KUOVATEKI...KUMBUKA HILI!



No comments:

WATEMBELEAJI