UJENGAJI WA PAMPU YA KUVUTA MAJI KWA KUTUMIA UPEPO!
Hapa tukipandisha injini yake juu...ni nzito balaa, ni wakati pekee tunapovaa mikanda ya kulinda usianguke, la sivyo katika matengenezo ya kawaida huwa tunapanda hivyo hivyo kwa mazoea pia kwa uangalifu sana, maana ukianguka ndio mwisho wako, mimi nilizoea sana kazi hizi nilikuwa napanda kama nyani, wakati mwingine na vitu vizito kwenda navyo juu kubadilisha katika matengenezo. Kwakweli kama una kizunguzungu hapa huwezi kupanda, maana ni juu sana kilele chake.
Vijana kutoka Canada, wakishangaa kwa kutazama juu jinsi linavyosukwa Windmill kwaajili ya kuvuta maji kwa njia ya upepo. Tuliogopa kuwapandisha juu, maana ni juu sasa lazima uwe mzoefu. Zamani nilikuwa napanda kama nyani, lakini siku hizi nimepunguza...labda na uzee unanyemelea kidogo kidogo, lakini bado napanda na kufanya kazi kama kawaida.
Ujengaji wa Pampu ( WINDMILL) ya kuvutia maji kisimani kwa kutumia upepo, maana huko vijijini hakuna umeme...kwahiyo Windmill inakuwa msaada mkubwa sana kuvuta maji, baada ya kuchimbwa kisima huwa kazi inayofuatia ni kujenga jamaa hili. Ni kazi ngumu sana kulijenga hili dude, maana ni refu sana kwenda juu vyuma vyake ni vizito sana inahitajika nguvu ya kutosha, pia uwe umetulia na kichwa kama una kizunguzungu marufuku huwezi ni hatari sana.
No comments:
Post a Comment