Mpende Mkeo/Mmeo....uliye mchagua mwenyewe bila kulazimishwa na mtu yoyote. Pasipo shuruti ulijichagulia Mkeo/Mmeo, ulizidi upendo ndani ya ndoa ili watu waone, ulizidi upendo ili watu wajifunze kutoka kwenu, sasa msiruhusu malumbano ndani ya ndoa.
Mahali ulitoa na wao wakapokea; hivyo mjengeane heshima wenyewe kwa wenyewe, mtaheshimika machoni kwa watu na hata kwa watoto wenu. Pendaneni ili watu waige kwenu.
Watu wote waliohudhuria ndoa yenu ni mashahidi, mmeomba wenyewe mbele ya kadamnasi hivyo hamna budi kuyaishi haya.
Kuna kawaida ya wana ndugu kupendelea kuzivuruga ndoa, ole wenu siku hiyo mtajibu.
UTENDEE HAKI MOYO WAKO KWA KUMPENDA SANA MTU SAHIHI!
- Kila lakheri nyingi sana kwa wana ndoa wote duniani.
2 comments:
Mikimiki katika maisha ya ndoa imeendelea kuwa Tsunami ya Ulimwenguni na wadau wote wajitahidi kudumisha ndoa.
===================================
Ndoa na iheshimiwe kati ya wote, na kitanda cha ndoa kiwe bila unajisi, kwa maana Mungu atawahukumu waasherati na wazinzi._Waebrania 13:4
Mimi Nina tatizo kwa ndoa yangu mke wangu huchat na mwanaume wake wa zamani na nikimuonya hujibu"ndege wa kwako manati ya mini,Niko kwako na ukitaka tuishi wacha simu yangu ama nikikua nitaacha"hili jambo wazazi wangu wameanza kuigilia na kudai Mimi ndo mbaya tena Nina hasira na kudai watanifukuza nyumbani hadi Mimi humfumania akiongea nae Kwa simu na huikata na ku sms kisha aizime kabisa naombeni mawazo
Post a Comment