
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia mwishoni mwa wiki, katika Kijiji cha Nyaruguguna, Kata na Tarafa ya Nyang'hwale ambapo mlemavu huyo, Adam Robert(14) mwanafunzi wa darasa la nne, alivamiwa na kukatwa mkono wa kushoto.
Ni jambo la kusikitisha sana kuona vitendo hivi vinaendelea kutokea, na mwisho wa siku Jeshi linataka kutumia fedha za walipa kodi kwa ajili ya kuwapa wahalifu hao, mi nadhani hii njia sio sahihi, sidhani kama Jeshi la Polisi wanashindwa kuwapata hawa wanaowatuma wahalifu kwenda kuwadhuru Maalbino hawa. Jambo la msingi hapa sio kutangaza dau ni kuhakikisha wale wanaowatuma ndio wanakamatwa na ninaamini Jeshi la Polisi likishirikiana na Usalama wa Taifa inawezekana kuwakamata hawa na kuwatokomeza kabisa, usalama wa Taifa wanafanya kazi gani kama sio pia na kuangalia usalama wa Watanzania hawa?
Ni aibu kubwa kwa Taifa letu, kwa vitendo hivi vinavyoendelea.
- Mdau Henry Kapinga.
No comments:
Post a Comment