Thursday, October 13, 2011

BABA WA TAIFA LETU......TUNAKUKUMBUKA SANA DAIMA!

Leo tunakumbuka siku yako ulipotutoka hapa duniani.....lakini pamoja na kifo kukuchukua, ila sisi tupo pamoja nawe daima siku zote! Tunakukumbuka sana Baba yetu mpendwa, kwa mazuri uliyo lifanyia Taifa hili.....hasa kabisa Umoja na Amani ulivyo tuachia, huu ni utajiri mkubwa sana katika Taifa letu zaidi ya utajiri wowote ule, ukizingatia Mataifa mengine wanapigania kila kukicha ili wapate vitu hivi viwili; Umoja na Amani....lakini hawavipati bado. Sisi Watanzania tunajivunia kwa sana tu, yote hii ni kwaajili yako wewe na mwenzio Karume....tutawakumbuka daima. Mpaka sasa watu wa Utandawazi; bado hawajagundua njia ya kuwasiliana na watu muhimu kama nyinyi mliopo huko mbinguni kwa Mungu Baba......lakini naamini kabisa ujumbe wetu utaupata tu kuwa; tunakumiss sana tu sisi wanao Watanzania, na kukujali mno kupita kiasi. Wape salamu na Waasisi wenzako wote huko mlipo walio kusaidia kwa hali na mali kuupigania Uhuru wetu.
-Blog hii inakusalimu sana na kukuenzi kwa sana....na itaendelea kukuenzi daima! Tunakumiss sana Baba, na Mwenyezi Mungu azidi kukupa pumziko la milele...amina!

No comments:

WATEMBELEAJI