Thursday, October 13, 2011

TUKIPITA KIJIJINI....MARA TUNAKARIBISHWA SHEREHENI!



Mara tukakaribishwa kwa masista katika kupata chakula, bila kutegemea kabisa tulikuwa wapitaji njia tu, katika kushangaa kijiji changu nilipo zaliwa. Wageni wangu walishangaa sana na kusema; kwakweli Watanzania ni wakarimu sana, wewe mwenyewe unafahamu Ulaya jinsi tulivyo kila kitu kinaenda kwa mahesabu....ni sababu za uchoyo tu hakuna lolote, walisema hivyo wageni hao....na kufurahi sana.
















Wana TYCS...MAPENDO DAIMA!









Mimi na wageni wangu kutoka Italy, tulikuwa tukipita Kijijini kwangu kusalimia...mara tunakuta sherehe ya wanafunzi wa Kidato cha nne wakiagwa..... Wana TYCS. Mara tukaaliwa na sisi, hamna kupita bila kuhudhuria sherehe ni lazima alisema hivyo Headmaster, huko kijijini wanapenda sana wageni. Sherehe ilikuwa nzuri ya kupendeza bila mambo mengi na madoido ya ghalama, sherehe ya kiaina tu lakini inafurahisha sana, wanafunzi jinsi walivyokuwa wamejiandaa kwa michezo mbalimbali ya kufurahisha mpaka basi. Wageni wangu walifurahi sana na kupiga picha kwa wingi.










No comments:

WATEMBELEAJI