Monday, October 24, 2011

KWAHERI MARCO SIMONCELLI.....ULALE SALAMA!

Msiba mkubwa uliotanda na huzuni nzito katika ulimwengu wa Sport hapa nchini Italy, baada ya kutokea ajali mbaya hapo jana huko nchini Malesia. Ajali hiyo ilimhusisha kijana Marco Simoncelli.....mwendesha pikipiki wa Kimataifa katika mashindano ya MOTO GP, ambapo alipoteza maisha yake katika ajali mbaya sana. Nchini Italy wanamlilia sana kijana wao mashuhuru sana katika michezo hii, ni msiba mzito sana katika nyaja za michezo hapa Italy. Alizaliwa katika mji mdogo wa Coriano - Cattolica (Rimini), ni jirani sana na hapa ninapoishi Cesena....hivyo ni huzuni sana katika miji ya hapa jirani. Alikuwa ni kijana mwenye sifa sana katika maisha yake ya michezo na pia maisha ya kawaida, mwenye kupenda kucheka na kuchekesha sana....hasa mimi nilikuwa nacheka sana wakati alipokuwa akihojiwa kwenye TV kutokana na rafudhi yake ya kabila la Waromanyoro, yaani ni watu wa maeneo ya hapa niishipo. Pia nilikuwa nampenda sana kutokana na kuwa mshangiliaji (mshabiki) sana wa Timu ya AC.MILAN, ambapo pia mimi ni mshabiki sana wa Timu hii. Baada ya shindano hilo la Malesia...alikuwa amepanga kwenda kwenye mechi ya Jumatano ya keshokutwa ya Ac.Milan na Parma, na alikuwa tayari ana Ticket kabisa....lakini basi mauti yakawa yamemkuta hapo jana. Hapo kesho tunatarajia kupokea maiti yake ikitokea huko Malesi. Yaani nasikitika sana na kusema; Mungu ampumzishe mahali pema peponi Marco Simoncelli...amina!


Marco...akiwa katika pikipiki yake, katika mashindano.




Hapa Marco akieleza jambo....kwa furaha!






Baba mzazi wa Marco Simoncelli, akiweka mikono kichwani baada ya kupata taarifa kuwa mtoto wake amefariki, maana baada ya ajali walimkimbiza Hospitalini na Baba yake alibaki katika viwanja vya michezo hiyo ya kukimbia pikipiki. Huko nchini Malesia....hapo jana saa nne asubuhi.








Marco Simoncelli, akiwa na rafiki yake.






HII HAPA VIDEO YA; AJALI YA MARCO SIMONCELLI.






No comments:

WATEMBELEAJI