Mkoa wa Iringa mbali na kuwa miongoni mwa Mikoa ambayo huzalisha sana mazao ya chakula hasa mahindi, nchini mwetu.....lakini pia ni Mkoa umekuwa mbele kwa uzalishaji wa mboga mboga kama nyanya na vitunguu. Katika kipindi chote cha mwaka zao la nyanya limekuwa likipatikana katika maeneo mengi ya Mkoa huu hasa kando kando ya barabara kuu ya Iringa - Mbeya au Iringa - Morogoro.
Pichani ni wafanyabiashara wa nyanya na vitunguu katika eneo la Ilula, Mkoani Iringa....wakiwahudumia wasafiri waliosimama kwa muda na gari ili kujipatia mahitaji yao katika eneo hilo ambalo linazalisha zao hili kwa wingi, na idadi kubwa imekuwa ikisafirishwa Jijini Dar es salaam. Ndoo moja ya nyanya inauzwa kati ya sh.3000 - 4000/= huku vitunguu vinauzwa kati ya sh.6500 - sh.7000/=
- Picha na Father Kidevu.
No comments:
Post a Comment