Monday, October 17, 2011

RWANDA, BURUNDI NA TANZANIA.....KUJENGA RELI MPYA!

Bwana Albert Sengiyumva, Waziri wa miundombinu nchini Rwanda anasema kwamba; hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2011, Burundi, Rwanda na Tanzania....zitakuwa zimekwisha unda Sekretarieti itakayosimamia ujenzi wa reli mpya itakayohudumia nchi hizi kwa siku za usoni.
Itakumbukwa kwamba; Rwanda na Burundi ni kati ya nchi ambazo hazina bandari na hivyo zinalazimika kutumia Bandari ya Dar es salaam kwaajili ya kusafirishia mizigo yao.
Mradi huu utagharimikiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, na unatarajiwa kuwa na njia mbili za reli zenye urefu wa kilomita mia nne na tisini na nne (494). Bandari kavu ya Isaka, Tanzania itakuwa ni kiungo kikuu kati ya Tanzania, Rwanda na Burundi.

No comments:

WATEMBELEAJI