Thursday, November 24, 2011

AJALI YAWAPOTEZEA MAISHA WAMISSIONARI WA 3 WAKAPUCHINI.

WAMISSIONARI WATATU WAKAPUCHINI NA KIJANA MMOJA WAFARIKI DUNIA, ENEO LA RUVU....WAKIWA WANAELEKEA DAR ES SALAAM.


Wamissionari watatu wa Shirika la Ndugu Wadogo wa Mtakatifu Francisco - Wakapuchini pamoja na kijana mmoja wamepoteza maisha yao kutokana na ajali ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Kongwa - Dodoma, kugongana uso kwa uso na Lori...eneo la Ruvu kwa Zoka, Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani. Ajali hiyo imetokea siku ya Jumanne, tarehe 22 Novemba 2011.
Waliofariki dunia ni Padre Silverio Ghelli (73) Corrado Trivelli (77), Luciano Baffigi (64), pamoja na kijana Andrea Ferri. Wakapuchini hawa walikuwa wanatoka Parokia ya Kongwa, Jimbo Katoliki Dodoma, walikuwa wamekwenda kwaajili ya uzinduzi wa shule ya Awali inayoendeshwa na Shirika la Masista wa Upendo wa Bikira Maria mkingiwa dhambi ya asili la Ivrea.

Marehemu Padre Luciano Baffigi, alikuwa ni Mkuu wa Shirika la Wakapuchini Kanda ya Toscana - Italia, alikuwa kwenye ziara ya kichungaji nchini Tanzania kuanzia hapo tarehe 15 Novemba 2011, na kwamba alikuwa anatarajia kurudi Italia hapo tarehe 3 Disemba 2011. Lakini amekutwa na mauti akiwa njiani kuelekea Dar es salaam.

Padri Silverio Ghelli ni kati ya Wamissionari wa Kapuchini waliofanya utume wao nchini Tanzania kwa miaka mingi. Yeye alifariki hapo hapo kwenye eneo la ajali Ruvu, wengine watatu walifariki dunia wakiwa wanapelekwa Hospitalini - Kibaha. Padri Silverio hadi mauti yanamfika alikuwa ni Paroko msaidizi wa Parokia ya Pugu, Jimbo kuu la Dar es salaam.....lakini waamini na wananchi wa Dodoma wanamkumbuka sana kutokana na mchango wake mkubwa katika mchakato mzima wa uinjilishaji, uliokuwa unagusa mahitaji ya mtu mzima; Kiroho na Kimwili.

- Blog hii inatoa; Pole sana kwa Wamissionari wote Wakapuchini kwa kuondokewa na wapendwa wao, na Mwenyezi Mungu awalaze mahali pema peponi marehemu hawa....amina!

No comments:

WATEMBELEAJI