ALIWAPIGIZA CHINI WATALII......HATARI LAKINI SALAMA!

Wakati tunarudi kutoka Serengeti-Ngorongoro - Arusha, nikiwa na wageni wangu, tulikutana na hawa jamaa wakivutana.....baadae tulionana nao sehemu moja ya mapumziko kabla hujafika Arusha mjini. Jamaa walituhadithia kuwa dereva wa gari hili la Watalii alipinduka na gari hii na kuishia mitini (kukimbia), huku watalii wakiwa wameumia kiasi, lakini hakuna aliyepoteza maisha yake. Ukipewa kijana akuendeshe huko porini katika mambo ya utalii una kazi kweli kweli, ilishanitokea wakati fulani....maana wanakimbia sana tena wakisikia kwenye radiocall zao kuwa kuna mnyama mahali, hapo ushike roho mkononi, maana wanaambizana kwenye radio; kuna Simba aka Sharubu sehemu basi wote hukimbilia huko ili wageni waone. Vijana hawa machachari wanayatupa magari kila mara kwa mwendo wa kasi ukizingatia barabara ya mbugani ni mbaya sana. Vijana hawa wanaitwa kwa jina la utani; Serengeti Boyz, mara ya mwisho nilikuwa na mzee wa makamo yeye ni mstaarabu sana katika kuendesha, ikitupita tu gari kwa mwendo wa kazi utasikia; SERENGETI BOY HUYO......hatari lakini salama!
No comments:
Post a Comment