Askofu Mkuu Francesco Montecillo Padilla, balozi mpya wa Vatican nchini Tanzania.
Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, Alhamisi tarehe 10 Novemba, 2011 alimteuwa Askofu Mkuu Francesco Montecillo Padilla kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Tanzania. Kabla ya uteuzi huu, Askofu Mkuu Padilla alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Papua New Guinea na Visiwa vya Solomoni.
Askofu Mkuu Francesco Montecillo Padilla alizaliwa kunako tarehe 17 Septemba, 1953 huko Cepu, nchini Ufilippini. Baada ya masomo na majiundo yake ya kipandre, alipadirishwa kunako tarehe 21 Oktoba, 1976. Aliwekwa wakfu kuwa Askofu kunako tarehe 23 Mei, 2006. Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Askofu Mkuu Joseph Chennoth aliyeteuliwa hivi karibuni na Baba Mtakatifu kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Japan.
No comments:
Post a Comment