Monday, November 14, 2011

KARUME NA NYERERE......WAENZIWE KWA VITENDO!





















Waasisi wa Muungano wa Tanzania, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Karume, wanapaswa kuenziwa kwa vitendo ili kuharakisha maendeleo ya Kijamii, Kisiasa na Kiuchumi.

Waasisi hawa wanastahili heshima ya pekee kutokana na jitihada zao za kusimamia haki na kuimarisha misingi ya utawala bora.....ambao ni nguzo za maendeleo katika Taifa lolote duniani.

Dunia inatambua mchango wa Waasisi hawa katika kupigania uhuru na kuunganisha Muungano ambao umepata mafanikio makubwa. Ki msingi tuatambua na kuheshimu mchango mkubwa waliotoa enzi ya uhai wao na tutaendelea kuwakumbuka daima!


Huwezi kuadhimisha miaka 50 ya Tanzania bila kuwataja Waasisi hawa ambao walishirikiana katika mambo mengi ya msingi, ambayo leo hii matunda yake yameanza kuonekana kwa Watanzania wote. Amani, Umoja na Utulivu uliopo Tanzania ni matunda ya Wazee hawa kutokana na jitihada zao za kuimarisha misingi ya utawala bora.


- Watanzania tunajivunia mambo mengi ambayo yametokana na busara za Wazee hawa Karume na Nyerere, ambao waliwapenda wananchi na kuwawekea misingi mizuri ya maisha bora ya amani na umoja. Kielelezo kuwa dunia inatambua mchango wa Waasisi hawa katika kuimarisha Umoja na Mshikamano wa nchi yao.









No comments:

WATEMBELEAJI