Tuesday, November 29, 2011

MISA YA MIILI YA MAPADRI WATATU NA KIJANA MLEI.

Mapadri wakiwa wamebeba moja ya majeneza yenye miili ya mapadri watatu na kijana mlei, wakipeleka kwenye gari kwenda kuhifadhiwa vizuri Hospitali ya agakhan kabla ya kusafirishwa kwenda Italia. Hapa baada ya kuiombea katika Ibada maalumu iliyofanyika jana Jumatatu katika Kanisa Katoliki Msimbazi - Dar es salaam...tayari kusafirishwa nchini kwao Italia kwa mazishi.
Mapadri hawa walikufa katika ajali ya gari, waliokuwa wakisafiri kutoka Kongwa - Dodoma kwenda Dar es salaam, tayari na safari ya kurudi kwao Italia...lakini bahati mbaya mauti yakawakuta katika ajali hiyo. Ajali hiyo ilitokea tarehe 22 Novemba 2011 katika eneo la Ruvu - Mkoani Pwani.....baada ya kugongana uso kwa uso na Lori.

Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es salaam, Salutaris Libena....akiongoza Ibada ya maombezi ya miili ya Mapadri watatu na kijana Mlei mmoja, katika Ibada maalumu iliyofanyika jana Jumatatu Msimbazi - Dar es salaam.



Masista wakiwa na nyuso za huzuni sana....katika Ibada ya kuwaombea Marehemu Mapadri Wakapuchini.






Baadhi ya Waumini wakilia wakati majeneza yenye miili ya Mapadri na Mlei mmoja ikipakiwa kwenye magari baada ya kuombewa.






1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Marehemu wote wastarehe kwa amani mahali pema peponi. AMINA.

WATEMBELEAJI