Saturday, November 26, 2011

SALAMU ZA RAMBI RAMBI ZA RAIS KIKWETE KWA MAPADRI.

NDUGU WAFRANCISCANI WAKAPUCHINI WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA GARI NCHINI TANZANIA...KURUDISHWA WOTE KWA MAZIKO, ITALIA!


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Jakaya Mrisho Kikwete, ametuma salamu za rambi rambi kwa Padre Wolfagang Pisa...Mkuu wa Shirika la Ndugu Wafrancisko Wakapuchini, nchini Tanzania....kufuatia vifo vya Mapadre watatu na mlei mmoja, katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Ruvu kwa Zoka, Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani, Jumanne..tarehe 22 Novemba 2011.

Rais Kikwete, anasema katika taarifa yake hiyo kwamba; amepokea kwa masikitiko makubwa habari za vifo vya Mapadre Wakapuchini katika ajali ya gari. Anachukua fursa hii kuwatumia Wakapuchini wote salamu zake za rambirambi. Waliofariki dunia katika ajali hiyo ni: Padre Silverio Ghelli, Padre Corrado Trivelli, Padre Luciano Baffigi na Mlei Andrea Ferri.
Wakati huo huo, Mheshimiwa Padre Wolfgang Pisa...Mkuu wa Shirika la Ndugu Wadogo Wafrancisko Wakapuchini Tanzania, katika taarifa yake anasema kwamba; miili ya ndugu wote waliofariki dunia katika ajali hii itarudishwa nchini Italy kwa mazishi. Kardinali Polycarp Pengo, Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es salaam....anatarajiwa kuongoza Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kuwakumbuka na kuwaombea marehemu hao, Jumapili ya kesho jioni majira ya saa 10:30 katika Parokia ya Pugu, Jimbo kuu la Dar es salaam.

Baada ya Ibada hiyo ya Misa Takatifu, miili ya marehemu itapelekwa Parokia ya Msimbazi, Jimbo kuu la Dar es salaam, kwa maandamano na mkesha. Jumatatu asubuhi saa 4:30 kutakuwa na Ibada ya Misa Takatifu itakayoongozwa na Askofu Msaidizi Salutaris Libena wa Jimbo kuu la Dar es salaam. Askofu Mkuu Yuda Thadeus Ruwaichi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania. Pia yeye ni Mkapuchini, anatarajiwa kutoa mahubiri wakati wa maadhimisho hayo.
Baada ya maadhimisho hayo, miili ya marehemu itapelekwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, tayari kusafirishwa kwenda Italia kwa maziko. Kutoka Tanzania msafara huu utaongozwa na Ndugu Felician Kavishe, Makamu Mkuu wa Shirika la Ndugu Wafranciskani Wakapuchini, Tanzania. Kwa kipindi cha siku hizi, katika nyumba na Jumuiya za Wafranciskani kutakuwa na Misa na Ibada za maombolezo.



No comments:

WATEMBELEAJI