Sunday, November 27, 2011

TAFAKARI YANGU YA JUMAPILI HII NJEMA!

Ninapofikiri wema wako Mungu wangu, mimi mwenyewe ninajiuliza nitakupa nini? Ninawaza mimi.....ninawaza sana Mungu wangu; ninaleta sadaka yangu ndicho kipato changu ninaomba sana upokee!
Sadaka yangu ninayoleta mimi kwako, uibariki na kuitakasa. Vitu vyote vya duniani ni vyako, wewe unajua mimi nilivyo navyo vyote. Asante sana Bwana kwa mema yako yote kwangu mimi, sasa nakupa sadaka yangu ya leo.
- Neema zako siku zote zinanifaa....neema na vyote wewe umenipa kwa upendo!

No comments:

WATEMBELEAJI